Kuelekea msimu mpya wa EPL wikiendi ijayo, nyota wa Spurs, Harry Kane ameamua kusema ya moyoni baada ya varangati la siku chache.
Kane aliweka wazi adhma yake ya kutaka kuondoka Spurs kwenye dirisha hili la usajili lakini mambo yamekuwa tofauti. Kwa madai ya Harry Kane, alikuwa na makubaliano ya mdomo kati yake na mmiliki wa Spurs, Daniel Levy lakini amejikuta akiwekewa gharama kubwa kitu ambacho kinawashinda vigogo wa vilabu vinavyomtaka.
Kane alienda mbali zaidi kwa kutotokea mazoezini mapema wiki hii kama alivyotakiwa kufanya. Kitendo hiki kiliibua hisia za mashabiki wa Spurs, wadau wa soka na vyombo mbalimbali vya habari kuhusisha tukio hilo na matakwa ya Kane kutaka kuondoka Spurs.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Harry Kane ameamua kuweka chapisho ambalo limeelezea kwa ufupi hisia zake kwa kile kinachoendelea. Kati ya mengi aliyoandika, Kane amesisitiza kuwa hawezi na hana mpango wa kuvunja uhusiano wake na viongozi wa klabu, wachezaji wenzake na mashabiki ambao ndio watu muhimu zaidi kwenye maisha yake ya soka.
Kane ameongeza kuwa, atarejea mazoezini kama walivyokubaliana (leo). Man City wanahusishwa na kumtaka Kane lakini kama Spurs wataeka ugumu basi wataachana nae.
Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!



Sarah
Asante kwa taarifa