Mshambuliaji wa klabu Tottenham Hotspurs Harry Kane ameingia kwenye rada za klabu ya Manchester United kwa mara nyingine wakati huu klabu hiyo inatafuta mshambuliaji.

Klabu ya Manchester United ipo kwenye mkakati wa kutafuta mshambuliaji wa kudumu ndani ya klabu hiyo mwenye ubora wa kiwango cha dunia. Harry Kane anatajwa kua kwenye orodha ya juu kabisa katika majina yanayohitajika ndani ya klabu hiyo.Harry KaneManchester United imefanikiwa kukamilisha dili la mshambuliaji wa klabu ya Burnley aliyekua kwa mkopo kwenye klabu ya Besiktas Wout Weghorst raia wa kimataifa wa Uholanzi, Mshambuliaji huyo amesajiliwa kwa mkopo wa miezi sita mpaka mwishoni mwa msimu.

Baada ya kukamilisha dili la Weighorst klabu hiyo bado inafanyia kazi namna ya kumpata nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza ambaye amekua kwenye ubora wa juu kwa muda mrefu ndani ya klabu ya Tottenham na klabu hiyo imeona anaweza klua tiba na suluhisho kwenye eneo la ushambuliaji ndani ya klabu hiyo.Harry KaneGwiji wa zamani wa klabu hiyo Rio Ferdinand pia ameishauri klabu yake hiyo ya zamani kua kama inataka mshambuliaji ambaye atakidhi ubora ndani ya klabu hiyo basi jibu lao linapaswa kua Harry Kane. Na klabu hiyo inapanga kuandaa ofa kubwa ya kuweza kumshawishi nyota kuelekea majira ya joto mwezi Juni ili kuweza kunasa saini ya mshambuliaji huyo matata.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa