Havertz Arejea Kwa Kishindo Kuwasubiri Leeds

Kai Havertz baada ya kurejea kikosini kwa mara ya kwanza baada ya siku 357, nyota huyo wa Ujerumani aliacha alama nzito kwenye ushindi wa Arsenal dhidi ya Kairat Almaty kwenye Ligi ya Mabingwa, na sasa macho yote yanaelekezwa kwenye pambano la Premier League dhidi ya Leeds United Jumamosi.

Havertz, aliyekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha ya goti na misuli ya paja, alitumia nafasi yake kikamilifu. Akiwa ameanza mechi kwa mara ya kwanza tangu alipoanza kuuguza majeraha, alihusika moja kwa moja kwenye mabao yote matatu ya Gunners, akifunga mwenyewe na pia kumpasia Viktor Gyokeres pasi ya bao mapema dakika ya pili.

Havertz Arejea Kwa Kishindo Kuwasubiri Leeds

Baada ya kiwango hicho, Kocha wa Arsenal Mikel Arteta hakuficha kuridhishwa kwake. “Ubora aliouonesha, muunganiko wake na timu, bao alilofunga na asisti aliyotoa kipindi cha kwanza, yote hayo yalifanya uwe mchezo mzuri sana kwake,” alisema Arteta. Kilichovutia zaidi ni kwamba Havertz alicheza nafasi ya ndani zaidi ya kiungo, akionesha uwezo wa hali ya juu wa kiufundi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Ingawa alitolewa wakati wa mapumziko, Arteta alifafanua kuwa ilikuwa sehemu ya mpango wa makusudi. Dakika 45 zilipangwa ili kumjenga kimwili taratibu. “Tulipanga acheze dakika 45. Kuanzia sasa, tutalazimika kufanya maamuzi kama aanze au la kwenye mashindano yajayo,” aliongeza Arteta akimaanisha wazi kuwa nafasi ya kuanza iko mezani.

Havertz Arejea Kwa Kishindo Kuwasubiri Leeds

Kabla ya mechi hiyo, Havertz alikuwa amecheza dakika 59 tu msimu mzima. Lakini sasa, baada ya kuonesha njaa na ubora, Arteta anatarajia nguvu mpya. “Bila shaka alitaka kuendelea kucheza leo, kwa hiyo najua kitakachotokea kesho,” alisema kwa tabasamu. Swali sasa ni moja, je, Arteta atamjumuisha Havertz kuanzia mwanzo dhidi ya Leeds jumamosi hii au hapana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.