Ukraine Yamshambulia Infantino, Yadai Ana Kauli Za Kitoto

Mvutano mkubwa umeibuka kati ya Ukraine na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, baada ya kiongozi huyo wa soka duniani kupendekeza uwezekano wa kuondoa marufuku kwa Urusi katika mashindano ya kimataifa. Waziri wa Michezo wa Ukraine, Matvii Bidnyi, amemshambulia Infantino vikali, akimuita asiye na uwajibikaji na mwenye kauli za kitoto, akisisitiza kuwa soka haliwezi kutenganishwa na uhalisia wa vita vinavyoendelea.

Urusi ilisimamishwa kushiriki mashindano yote ya FIFA na UEFA tangu Februari 2022 kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine. Hata hivyo, Infantino amesema marufuku hiyo haijafanikisha chochote bali imezalisha hasira na chuki zaidi, akidai kuwa kuruhusu watoto wa Urusi kucheza soka Ulaya kungeleta mwelekeo chanya. Kauli hizo ndizo zilizomchochea Bidnyi kujibu kwa ukali kupitia mitandao ya kijamii.

Ukraine

“Maneno ya Gianni Infantino yanasikika kuwa hayana uwajibikaji, kama si ya kitoto kabisa,” alisema Bidnyi. “Yanalitenganisha soka na uhalisia ambao watoto wanauawa. Tangu mwanzo wa uvamizi kamili wa Urusi, zaidi ya wanamichezo na makocha 650 wa Ukraine wameuawa, wakiwemo zaidi ya wachezaji 100 wa soka.” Kauli hiyo imeongeza uzito wa mjadala juu ya nafasi ya michezo wakati wa vita.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Ukraine

Bidnyi pia alisisitiza kuwa vita si siasa bali ni uhalifu, akilaumu Urusi kwa kutumia michezo kama chombo cha kuhalalisha uchokozi. Aliongeza kuwa Ukraine inaungana na msimamo wa Shirikisho la Soka la Ukraine kupinga kurejea kwa Urusi katika mashindano ya kimataifa, akisema bendera na alama za taifa hilo hazina nafasi katika michezo inayoheshimu haki, uadilifu na fair play wakati mauaji yanaendelea.

Ukraine

Licha ya marufuku, Urusi imeendelea kucheza mechi za kirafiki dhidi ya mataifa yasiyo ya Magharibi bila ruhusa ya FIFA au UEFA. Hata hivyo, imekosa kushiriki Kombe la Dunia 2022, Euro 2024, na haitakuwepo Kombe la Dunia 2026. Pia, Ukraine iliwahi kuukosoa vikali uamuzi wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Walemavu (IPC) kuondoa marufuku kwa wanariadha wa Urusi na Belarus, ingawa bado hawatashiriki Michezo ya Walemavu ya Majira ya Baridi ijayo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.