Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Rasmus Hojlund leo atashuka dimbani kukabiliana na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Manchester City katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

Rasmus Hojlund mpaka sasa hajafanikiwa kufunga katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza akiwa amecheza michezo sita mpaka sasa, Hivo inasubiriwa kama ataweza kutamba katika mchezo dhidi ya Manchester City leo.hojlundMchezaji huyo ameshafungua ukurasa wake wa mabao katika ligi ya mabingwa ulaya ambapo mpaka sasa ameshapachika wavuni mabao matatu, Lakini kwenye ligi kuu ya Uingereza akiwa bado hajafanikiwa kufunga bao hata moja.

Mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Denmark amekua na mwanzo mzuri ndani ya kikosi cha Manchester United, Lakini sio kwenye ligi kuu ya Uingereza jambo ambalo linafanya mashabiki wa klabu hiyo kutokua na amani wakitaka afunge kwenye ligi kuu ya Uingereza.hojlundKuna wakati inatokea mchezaji hafanyi vizuri kwenye michuano fulani lakini anafanya vizuri kwenye michuano mingini, Vilevile hutokea mchezaji kuibukia kwenye mchezo mkubwa hivo Manchester derby inaweza kua sehemu ya kumfufua Rasmus Hojlund na kuanza kufunga kupitia mchezo huu.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa