Maisha ya nyota wa Argentina, Mauro Icardi ndani ya Inter Milan, huenda yakafikia ukingoni msimu huu, baada ya Makamu wa Rais wa timu hiyo, Javier Zanetti, kudai kuwa hadhani kama nyota huyo ana maisha tena ndani ya Inter.
Icardi aliingia kwenye mgogoro na viongozi wa Inter Milan pamoja na mashabiki mwaka jana, jambo ambalo lilisababisha apokonywe unahodha na kupelekwa kwa mkopo PSG ya Ufaransa.

Inaelezwa kuwa huenda PSG ikamsaini staa huyo moja kwa moja baada ya kuifungia timu hiyo magoli 20 na pasi nne za magoli katika mechi 31 alizocheza msimu huu.
Chelsea na mabingwa wa Italia, Juventus wanatajwa kuwania saini ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 27, na tayari mke wake, Wanda amedai kuwa wanaweza kurejea Italia.


Franky
Maoni yangu bola haende PSG tu at a kwa mkopo