Kocha mkuu wa Intermilan Simone Inzaghi anatamani timu yake irejee kwenye mstari mzuri ambapo wamekuwa na matokeo ambayo hayaridhishi wanayoyapata kwenye michezo ya hivi karibuni toka ligi irejee.

 

Inzaghi Kupunguza Presha Inter

Inzaghi anatarajia kufanya vizuri kwenye mechi ya leo dhidi ya Torino ambapo watakuwa nyumbani ili kupunguza presha waliyo nayo kitu ambacho kinawafanya wasiwe na mwendelezo mzuri katika mechi yao.

Kipigo walichopata cha mabao 3-2 kwenye mchezo wao Dabi dhidi ya AC Milan kiliwafanya washuke hadi nafasi ya 8 kwenye msimamo wa Serie A, baada ya mechi tano na wakafuatia kichapo hicho kwa kuonyesha kiwango duni kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich, na hatimae kufungwa kwa mabao 2-0 wakiwa San Siro.

 

Inzaghi Kupunguza Presha Inter

Mabingwa hao wa msimu juzi wa Serie A wameanza vibaya msimu wa klabu bingwa huku wachezaji watatu wa safu ya ulinzi Milan Skrinar, Stefan De Vrij na Alessandro Baston wote wamekuwa sio wa kutegemewa mwezi wa msimu huu huku utegemezi mkubwa ukiwa ni kwa Dzeko mwenye umri wa miaka 36.

Huku kwa upande wa Torino wao walianza msimu vizuri, ingawa walipata kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Atalanta mapema mwezi huu, ambapo waliibuka mapema tena kwa Leece ambapo walishinda kwa bao moja kwa bila huku ushindi huo ukiwa ni wa tatu kwao baada ya kukutana na Monza na Cremonese.

 

Inzaghi Kupunguza Presha Inter

Presha inazidi kuwa kubwa Inzaghi kutokana na matokeo mabaya wanayopata na kukosekana kwa Romelu Lukaku katika eneo la ushambuliaji inafanya wapitie wakati mgumu, ambapo anabaki na Lautaro Martinez, na Joaquin Correa katika eneo hilo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa