Jude Bellingham alitangaza ubabe wake dimbani kwa kufunga bao katika mechi ya kwanza iliyoshuhudia waajiri wake Borussia Dortmund katika ushindi mnono wa 5-0 dhidi ya MSV Duisburg katika raundi ya kwanza ya German Cup.
Bellingham, 17, alisajiliwa na Dortmund kutoka Birmingham City kwa kima cha £22.75m mnamo Julai 2020.

Mnamo Agosti 2019, kinda huyo alivunja rekodi ya mvamizi wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Trevor Francis kwa kuwa mchezaji mchanga zaidi kuwahi kuwajibishwa katika kikosi cha kwanza cha Birmingham akiwa na umri wa miaka 16 na siku 38 pekee.
Jadon Sancho aliwafungulia Dortmund ukurasa wa mabao kupitia penalti ya dakika 15 kabla ya Bellingham kufanya mambo kuwa 2-0 katika dakika ya 30.
Kadi nyekundu ambayo Dominic Volkmer wa Duisburg alionyeshwa ililemaza kabisa uthabiti wa wenyeji wa Dortmund ambao walifungiwa mabao mengine na Erling Braut Haaland, Gio Reyna na Marco Reus katika dakika za 39, 50 na 58 mtawalia.

Licha ya Sancho kuhusishwa na uwezekano mkubwa wa kutua Man-United, Dortmund wamesisitiza kwamba Mwingereza huyo atasalia Signal Iduna Park hadi timu inayomtaka iweke mezani kima cha £120m ndipo washawishike kumwachilia.
Mabao kutoka kwa Sancho na Bellingham yalimaanisha kwamba wanaweka historia ya katika kikosi cha Dortmund kuwa wanasoka wawili raia wa Uingereza kuwahi kupangwa katika kikosi cha kwanza na kila mmoja wao kufunga bao.
Goli la Bellingham lilimweka katika historia ya miaka 110 ya Dortmund kwa kuwa mwanasoka mchanga zaidi kuwahi kufungia bao miamba hao wa soka ya Ujerumani.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Adelta
Bellingham Ni mwenye history nzuri kwa wanasoka ujerumani#meridianbettz
Mwanahamisi
Ni historia nzuri kwa wanasoka
Elika
Khaaa kijana yuko vizuri sana
Zeiyana
Kujituma kwake Sancho ndio kuna pelekea vilabu vingi vikimtolea macho
Dorophina
Jude yupo vizuri sana mchezaji bora kwao
Caroline
Hongera zake
Fatina
Ni historian nzur kwa cc wapenda soka!
magdalena
kijana yupo vizuri katika kufunga ndo maana anatamba anajiamini sana
Mwajumah
Ni historia nzuri kwa wanasoka
aisha
Jude namkubali sana yuko vizuri
Nasra
Hongera sana
Angelina
Jude anastahili sifa ni mchezaji mzuri
Sabrina
Hongera sn
Neema
Hongera yake
Shafii
Gud news
Salma ngende
Kijana yupo vizuri
Rama
Yuko vizuri sana kijana
Shani
Zao lingine la dortmund hapa jude hapa haaland uwez kutoka
Sauda
Kijana anajua sana
Samira
Juhudi zake ndio zinamfanya anazidi kuwa kiungo bora zaidi
Janeflora malisa
Pongz kwake
Saupha mohamed
Hongera sana
Fatuma kasomo
Gud news
Hopemwaikuka
Kwa raha zake
Gabriel
Jude Bellingham yuko vzur sana
Frank P
Scouting ya dortmund iko vizuri sana
Samiah
Kwa raha zake
Khadija
Kijana yupo vzr sana#meridianbettz
Amiri Kayera
Atafk mbar dogo akikaza
Rose kapinga
Kazi nzuri
Issa
Pacha wa haaland dortmund
Theonestina
Namkubar Sana uyo jamaa
Genia Sikaluzwe
Hongera Sana kwa kipaji ulichonacho kijana
Theckla
Asante kwa taarifa
Rehema
Good
Furahav
Yuko vizuri
Ester jackson
Safiiiiii
Ernest
Jude Bellingham ameanza vizuri ndani ya Dortmund na kuweka historia yake kubwa katika club ya Dortmund
felister
atafika mbali akikaza
Tatu
Jude ni kijana Mdogo mchezaji mzuri anayekuja kwa kasi kwenye ulimwengu huu wa kandanda na anayejituma kwa juhudi zake anaweza kufika mbali
Lydia Emmanuel Magoti
Kijana Anajua kazi yake yupo vizuri kwenye kisoka
farida ahmadi
Kijana Yuko vizuri
marry
nice
David Pere
Scouting ya dortmund iko vizuri sana
Povel
Congrat kwake