Juventus ni mabingwa wa kombe la ligi nchini Italia kwa mara nyingine tena. Wababe hao wa soka nchini Italia wameweza kunyanyua ndoo hiyo ya ubingwa wakiwa bado na mechi za kutosha mkononi kwenye hatua ambayo ni mafanikio makubwa kwa klabu hiyo kongwe. Wamekuwa wa kwanza kati ya klabu nyingine ambazo nafasi yao bado haieleweki kama ni lini watanyanyua ndoo hiyo.
Kwa mwaka wa nane mfululizo wameshinda taji hilo la Serie A lakini kwa historia yao ya msimu huu ni jambo ambalo wamelifanya kama historia kabisa kwenye maisha ya klabu yao. Wamechukua ubingwa huo huku wakiwa wamepoteza michezo miwili pekee na mingine kuondoka na ushindi ama kusuluhu.
Katika hatua hizo nyota wao wa klabu hiyo alipumzishwa kwenye mechi mbili pekee ambazo ni ile ya SPAL na Genoa lakini ameweza kutumikia mechi nyingine zote na matunda yake ya usajili yameonekana dhahiri kabisa kwamba bado ana uwezo wa kufanya makubwa hata kwa umri wake.
Napoli pekee ndiyo wanamfuatia Juventus wakiwa nafasi ya pili lakini nafasi yao bado haijaweza kufua dafu mbele ya vinara hao ambao pamoja na uwezo wao bado hawajaweza kumfikia na hata kwa mechi hizo sita zilizobakia hawawezi kabisa kumfikia bingwa huyo. Hivyo, haikuwa na budi kutawazwa kama bingwa.

Kutua kwa Ronaldo kwa nafasi fulani kumeamsha ari ndani ya kikosi hicho hasa upande wa ligi lakini upande wa pili ambao ni wa klabu bingwa umeweza kuwa wa kawaida sana na haijaonesha ushawishi mkubwa sana na wenye upekee kwa sababu wametolewa kwenye hatua ya robo fainali ya michuano.
Vipi wengineo?
Ushindi huo wa mara ya nane mfululizo ni wa pekee kwa Juventus na hata kwenye ligi kubwa tano duniani. Wakifuatiwa na Lyon ambao wana historia ya kufanya hivyo mara saba mfululizo kwenye misimu ya 2001/2 na 2007/8 kukiwa hakuna klabu yoyote ya ligi hiyo ya Italia iliyowahi kuchukua ubingwa ikiwa imebakisha mechi tano mkononi.
Klabu nyingine zilizowahi kufikia hatua kama hiyo ni; Bayern Munich ikiwa chini ya Pep iliweza kutangaza ubingwa baada ya mechi zake 27 pekee kwenye msimu wa 2013/14, PSG nao waliweza kufanya hivyo baada ya kushinda mechi zao 27 za ligi kwenye msimu wa 2015/16 huku Zlatan akiweka rekodi kwenye msimu huo.
Wengine ni Manchester United chini ya Ferguson, Barcelona nao wanaonekana kufanya hivyo ndani ya msimu huu ikiwa ni hatua kubwa kwao na watautwaa ubingwa wao wakiwa wamesalia na kama mechi nne mkononi; nao Inter Milan msimu wa 2006/7 chini ya Mancini walifanya maajabu hayo ya kunyakua ubingwa kabla ya mechi kumalizika zote.


Neema juma
Asante kwa kutujuza #meridianbet