Hii itakaa kwenye historia ya kila mpenda soka na shabiki wa klabu kama Arsenal, Leicester na Manchester United. Ni wikiendi iliyotawaliwa na matokeo mabovu kwa klabu hizo kubwa ambazo kwa hakika zilikuwa na nia ya kufanya vizuri ili ziweze kupanda na kujihakikishia nafasi kubwa ya kukaa nafasi nne za juu za ligi.
Mechi ilianza alasiri kabisa ambapo Goodison Park kuliwaka pale Everton walipowakaribisha Mashetani Wekundu na kushuhudia kichapo cha msimu kikiwatokea United ambao walionekana kama hawapo mchezoni kwenye mechi hiyo ambayo kwa hakika ilikuwa haina mvuto kwa upande mmoja.
Ilikuwa ni dakika za mapema sana ambapo Everton waliwakaribisha vizuri United ambapo nyota wa klabu hiyo anayefanya vizuri na miamba hao, Richarlison alipofungua karamu ya magoli ikiwa ni dakika ya 13 tangu mechi hiyo ianze. Mambo yakaonekana kama yatabadilika dakika za mbeleni lakini haikutokea hivyo baada ya Sigurdsson kuandika goli jingine kipindi cha kwanza hicho hicho dakika ya 28.
Kwa hakika wenyeji walionesha ubora wa aina yake kwenye mechi yao hiyo ikiwa ni ushindi mkubwa kwao kuupata mbele ya klabu kubwa zinazoshiriki ligi kuu.

Hata baada ya kipindi cha pili mambo yalizidi kuwa magumu upande wa United ambao hawakuonekana kabisa kusumbua safu ya ulinzi ya Everton na baadaye kuongezwa goli jingine ambalo lilitokana na uzembe mkubwa uliofanyika kwenye safu ya ulinzi na kumfanya Digne kuandika bao la tatu.
Adhabu haikuishia hapo hata baada ya kufanya mabadiliko na Walcott kuingia uwanjani alikuja na bahati yake na kufanikiwa kushindilia msumari mwingine ambao ulikamilisha hesabu ya goli nne ambazo United alizipokea bila kuwa na majibu ya aina yoyote ile ndani ya mechi hiyo.
Safari ya kufungwa kwa klabu kubwa haikuishia hapo; mechi nyingine iliyoshuhudiwa ni ile iliyokuwepo kati ya Arsenal ambao walikuwa wenyeji wa mechi hiyo dhidi ya Crystal Palace ambao walicheza soka safi na la kuvutia na kufanikiwa kuitingisha ngome ya Arsenal.
Walikuwa ni Benteke, Zaha na McArthur waliowapa adhabu Arsenal ambao kwa hakika mashahiki zao waliwapigia kelele United baada ya kupoteza hiyo ni kutokana na utani wa jadi uliopo kati ya wawili hao lakini ikakumbukwa kwa ule msemo usemao, “Hujafa hujaumbika” kwa kile kilichowakuta.
Baada ya matokeo hayo hakuna kitakachobadilika kati ya wawili hao zaidi ya mechi ya Chelsea inayosubiriwa japo atakuwa mbele kwa mchezo mmoja.


Furahav
Mpira hauna mwenyewe
Povel
Wadau wamechana Sana mikeka
Nasra
Mpira haujitaji ujuaji
Zeiyana
Kweli mpira hauna mwenyew