Kane Awaka Spurs Ikiua

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Kane ametakata katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Nottingham Forest huku klabu yake ikipata alama tatu muhimu wakiwa katika dimba lao la nyumbani.

Harry  Kane amefanikiwa kufunga mabao mawili katika mchezo wa leo dhidi ya Nottingham Forest huku Tottenham ikifanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja, Ikiwa ni baada ya kutoka kupoteza mchezo katika ligi hiyo wikiendi iliyomalizika dhidi ya Wolverhampton.kaneMshambuliaji huyo sasa ni kama anakimbiza mwizi kimyakimya kwani baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo amefikisha jumla ya mabao 20 katika ligi kuu ya Uingereza, Hivo sasa anakua amebakisha mabao 7 kumfikia kinara wa mabao mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Earling Haaland mwenye mabao 27.

Harry Kane amekua na ubora mkubwa sana ndani ya ligi kuu ya Uingereza kwa miaka takribani tisa sasa akifanikiwa kutwaa kiatu cha mfungaji bora wa ligi mara tatu, Hivo ni mchezaji ambaye tayari ameshajiweka kwenye daraja lake kutoaka na uwezo wake.kaneMshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekua akiwindwa na vilabu mbalimbali barani ulaya ikiwemo klabu ya Manchester United ambayo inaripotiwa kumuweka kwenye mipango yake kuelekea dirisha kubwa la usajili majira ya kiangazi, Kutokana na ubora ambao anauonesha ndani ya Spurs ni wazi kama atajiunga na Man United ataenda kufanya makubwa klabuni hapo.

Acha ujumbe