Klabu ya Chelsea sasa ni kama gari limewaka baada ya kupata alama tatu muhimu katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya Leicester City katika dimba la Kingpower kwa jumla ya mabao matatu kwa moja.
Klabu ya Chelsea baada ya ushindi wa leo wanafanikiwa kushinda michezo mitatu mfululizo baada ya kipindi kirefu, Klabu hiyo baada ya kuifunga Leeds katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza wikiendi ilyomalizika walifanikiwa kushinda mchezo dhidi ya Borussia Dortmund kwenye ligi ya mabingwa ulaya na leo unakua mchezo wa tatu mfululizo.
Vijana wa Graham Potter leo wametoa adhabu wakiwa ugenini katika dimba la Kingpower magoli ya Ben Chilwell, Kai Havertz na kiungo Matteo Kovacic yaliiwezesha klabu hiyo kupata alama tatu muhimu leo, Huku bao pekee la klabu ya Leicester City likifungwa na mshambuliaji Patson Daka.
Klabu ya Chelsea baada ya kufanikiwa kupata alama tatu leo dhidi ya Leicester City wamefanikiwa kufikisha jumla ya alama 37, Huku wakiendelea kukaa katika nafasi ya kumi kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakizidiwa alama moja na Brentford wanaokamata nafasi ya tisa.
Chelsea imeanza kuonesha uhai na kufufua matumaini ya kuitafuta nafasi ya kufuzu ligi ya mabingwa msimu ujao, Kama klabu hiyo ikiendeleza moto ambao imeuanzisha kwasasa basi ni wazi mabingwa hao wa zamani wa ligi ya mabingwa ulaya wanaweza kupata nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa ulaya.

