Karim Benzema Aongeza Mkataba Mpya

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema imeripotiwa amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Real Madrid mpaka mwaka 2024.

Kupitia kocha wa klabu ya Real Madrid ambaye amethibitisha kua Karim Benzema ataendelea kua sehemu ya kikosi cha mabingwa hao watetezi msimu ujao akizungumza na wanahabari Ancelotti alisema ” Karim ataendelea kua namba 9 wetu kwa msimu mwingine tena na kuendelea kufanya mambo makubwa kama kawaida”benzemaMshambuliaji huyo alikua anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu lakini taarifa zinasema mchezaji huyo ataendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwisho wa msimu wa 2023/24 ambapo mkataba wake ndio utakua uamalizika tena.

Klabu ya Real Madrid imekua inawaongezea mikataba mifupi wachezaji wake ambao wamekua wanafikisha umri wa miaka 30, Hivo ndio sababu ya Benzema pia kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja kwakua mchezaji huyo ana umri wa miaka 36.benzemaKlabu ya Real Madrid baada ya kumalizana na Benzema inaelezwa kwasasa ipo kwenye hatua za mwisho za kumuongezea mkataba mpya kiungo wake Luca Modric, Lakini pia wanamshawishi Toni Kroos ambae amepanga kustaafu wamuongeze mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kusalia klabuni hapo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.