Karim Benzema Apewa Nafasi ya Kujitetea Kasha ya Ulaghai!

Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Karim Benzema, atapewa nafasi ya pili ya kuthibitisha kutokuwa na hatia katika kesi ya ulaghai ya Mathieu Valbuena, baada ya adhabu kusimamishwa hapo awali.

Kesi hiyo iliyozua utata ikimuhusu mchezaji mwenzake wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, Valbuena, ambaye alidaiwa kukashifiwa baada ya mkanda wa ngono uliokuwa wa Valbuena kuangukia kwenye mikono ya matapeli.

Karim Benzema Apewa Nafasi ya Kujitetea Tena
Karim Benzema

Benzema amekuwa na msimamo wa kutokuwa na hatia tangu alipokamatwa kwa kesi hiyo, lakini mnamo Novemba alipewa adhabu ya faini ya Euro 75,000 na adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja iliyositishwa. Mshambulizi huyo wa zamani wa Lyon alipatikana na hatia hiyo, ingawa alikwepa kukaa gerezani wakati wowote.

Benzema ameendelea na majaribio yake ya kusafisha jina lake. Kama ilivyoripotiwa na ESPN kupitia Caught Offside, mahakama za Ufaransa zimempa rufaa ambayo itasikilizwa msimu huu wa joto.

Staa huyu alifukuzwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa kwa miaka saba kati ya 2014 na 2021, kabla ya kurejea chini ya Didier Deschamps kwa Euro 2021.


SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe