Baada ya Barcelona ya Messi kupokea kichapo cha aibu cha goli 8 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1946, Quique Satien na Barcelona bila shaka wanaenda kupeana talaka.
Satien, ambaye kikosi chake kimepokea kichapo cha 8-2 dhidi ya Bayern Munich, amesema kuwa Barcelona wanahitaji kurejesha heshima yao baada ya kuruhusu kichapo hicho kwenye Ligi ya Mabingwa.
Lakini ripoti zinasema kuwa meneja huyu, yuko mbioni kutimuliwa baada ya kile kilichotokea. Unafikiri ni wakati wake wa kufungasha vilago?
Kipindi cha kwanza pekee, kilitosha kuwavujisha jasho Barcelona wakienda mapumziko tayari wakiwa wamekubali bao 4-1, na goli 1 Bayern wakiwa wamejifunga. Ikumbukwe walikuwa wanaingia mechi hii wakiwa na hasira na majuto ya kuvuliwa ubingwa wa LaLiga na Real Madrid.

Mlinzi wa Barcelona, Gerard Pique ametoa wito kwa klabu kufanya mabadiliko katika nyanja zote za kikosi, unafikiri amegusia pia kuenguliwa kwa Meneja? 🤔
Satien, ambaye ambaye alichukua kibarua cha umeneja mikononi mwa Ernesto Valverde mwezi Januari amesema kuwa “Pique ni mchezaji ambaye amekuwepo hapa karibu maisha yake yote ya soka, mimi nimekuwepo hapa kwa miezi sita au nane, alichokiongea kinaingia akilini lakini mimi sio mtu sahihi wa kuliongelea hilo.”
Kichapo hiki kimewaumiza mashabiki wa Barcelona, maumivu haya yatachukua mda kupotea, lakini kibarua cha Satien kipo mashakani kwa sasa.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


Mwanahamisi
Asante kwa taarifa
aisha
Duuh pole sana kocha wa barcelona maana hicho sio kichapo kidogo kibongo bongo tunaita kichapo cha mbwa
Tatu
Hii habari mbaya Barcelona ya zamani sio ya sasa sio kwa kichapo kile anatakiwa kocha angalie wakae chini wajipange upya wakizubaa kichapo kile kile kitawafuata
warda
Kweli Maisha yanaenda kasi sana Barc wa kufugwa goli nane kweli?ha haaaaaaaa#Meridianbettz
Adelta
Duh pole Sana kocha wa Barcelona
@meridiabettz
Caroline
Kwa kweli ni aibu dahhh
Dorophina
Barca wameanza kutepeta sio kwa kichapo kile cha jana na Messi akiwepo ndani Barca na Messi wake saiz amna kitu
Mwajumah
Ni habari mbaya sana Barcelona ya zaman sio ya sasa sio kwa kichapo kile#Meridianbettz
Theckla
Kazi anayo kocha
Sylvester
Hii ilikua aibu kubwa sana kwa klabu kama Barcelona kutandikwa goli nane kwa mechi moja yani bora ingekua labda kuna home and away achapwe 4 alafu tena nne ila 8 kwa wakati mmoja duu,ina maana kungekuwa na home and away angechapwa magoli 16?Aibu sana hii lakini nayo inanikumbusha kipindi kile Arseanal alifungwa bila huruma goli 8 na Manchester Utd ila wao hawakufukuza kocha.Kocha wa Barcelona keshafukuzwa toka jana na ni muda muafaka sasa wa klabu kusukwa upya kwani enzi zakina Pique,Mesi zimeshaisha sasa..
Mariam mtandama
Daaah kama mpira wa mikono
Ernest
Sio tu Satien ila wachezaji wengi, Aksante kwa Countinho kwa kutunyoosha kisawasawa
Sadick
Quique Satien should go#meridianbettz
Lydia Emmanuel Magoti
Duu noma Sana Barcelona walicho kifanya Jana haibu kumfukuza kocha Satien sio ndio timu itakaa sawa akuna nimwelekeo wao aukukaa sawa huwanjani nivitu vyakukaa nakuongea kupanga tumekosea wapi namakosa yalekebishwe
felister
kweli zama zimebadilika
Shafii
Kwa matokeo hayo hata Mimi ningekua bosi ningekimbiza tu.
Zeiyana
Haibu kubwa kwa kweli clabu kubwa kama Barcelona kuchapwa magoli mengi kama vile mpila wa kikapu khaaa..!wamewashinda hata yanga
Samira
Afungashe tu virago aende Barcelona ni timu kubwa kwa kutoa matokeo ya jana ni fedheha kubwa timu
Neema
Duuu inahuzunishaaa kweli poleni Barcelona
Fatina mfingi
Hapo ndo unaambiwa mpira hautabiliki
Janeflora malisa
Dah kazi ipo jmn cocha
Gabriel
Barcelona jana walipoteana mapema sana hivyo kuwapa Bayern Munich uwaz mapema ila Kama wangejipanga mapema ile gem wangeweza kukabiliana nao kabisa kiukwel walionyesha udhaifu kwny mabek wa Kati na mbele kulikuwa vbaya kabisa
Rehema
Barua inakuusu kocha sio kwa aibu hiyo
Khadija
Asante kwa makala
Issa
Satien kubaki ni asilimia ndogo sana kwa kipigo cha jana kocha ndio atawajibishwa lakin ni wachezaji wenywe walipotea vibaya walizidiwa maarifa na bayern
Povel
Open door SATIen let go,🏃🏃🏃🏃🏃🏃
Saupha mohamed
Barcelona wameshinda sana sasaivi pia na mabeki hawana
Sabrina
Kazi ya ukocha ugumu wake upo hapoo anatakiwa afungashe kilicho chake akwende
Furahav
Daah ila ndo mpira hulvyo.
Hope mwaikuka
Hata m nisingeweza kwakwel ni aibu sana
Devotha
Daah! Ila Bayern wanasifa Sana hiyo ni komoa
Salma ngende
Tunao umia ni sisi mashabiki
Omary lukumbi
Hayo ndio maisha ukocha ukiwa kibaruan
Venerose
Barcelona wanatakiwa waongeze bidii katika mazoezi
Ester jackson
Kwa matokeo haya sidhani kama Luna viongozi watakao endelea
Rose kapinga
Kiukwel afanye aende tuu,maana ni aibu sana!!
David Pere
Hii ilikua aibu kubwa sana kwa klabu kama Barcelona kutandikwa goli nane kwa mechi moja yani bora ingekua labda kuna home and away achapwe 4 alafu tena nne ila 8 kwa wakati mmoja duu,ina maana kungekuwa na home and away angechapwa magoli 16?Aibu sana hii lakini nayo inanikumbusha kipindi kile Arseanal alifungwa bila huruma goli 8 na Manchester Utd ila wao hawakufukuza kocha.Kocha wa Barcelona keshafukuzwa toka jana na ni muda muafaka sasa wa klabu kusukwa upya kwani enzi zakina Pique,Mesi zimeshaisha sasa.kilichobakia kwao waende MSL tu
magdalena
barcelona kwa kichapo walichokipokea cha aibu sana yani wangepangua wachezaji wote na kukisuka upya kikosi icho ili wasijepokea tena aibu ya aina iyo
Omary lukumbi
Kweli kabisa imekua na matokeo mabovu mnoo