Klopp Ataka Mchezo wao na Spurs Urudiwe

Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp ametaka mchezo wao uliopigwa wiiendi iliyomalizika dhidi ya klabu ya Totenham Hotspurs kurudiwa kutokana na makosa yaliyofanywa na waamuzi.

Kocha Klopp anaona kua fidia ambayo itawafaa ni kurudia mchezo wao dhidi ya klabu ya Tottenham, Lakini tofauti na hapo sio jambo ambalo watakua wameridhishwa nalo kabisa.kloppKlabu ya Liverpool iliombwa radhi na chama cha marefa wa ligi kuu nchini Uingereza na hiyo ni baada ya kukatiliwa bao lao katika mchezo dhidi ya Tottenham lililofungwa na Luiz Diaz, Ambapo ilikuja kufahamika bao hilo lilikua halali na mchezaji hakuotea kama ambavyo ilitafsiriwa awali.

Kumekua na mvutano baada ya mchezo huo kwani mchezo huo pia ulikua na maamuzi ya kustaajabisha, Kwani klabu ya Liverpool ilipata kadi nyekundu mbili ambapo moja ya kadi hizo pia klabu hiyo wamelalamikia na kutaka kukata rufaa kwa madai haikua halali.kloppBaada ya chama cha marefa ligi kuu ya Uingereza kuiomba radhi klabu ya Liverpool kutokana na makosa yaliyofanyika katika mchezo wao ambayo waliyaita makosa ya kibinadamu, Lakini kocha Jurgen Klopp anaona fidia sahihi na itakayowaridhidha ni kurudia mchezo japo yeye mwenyewe anaona ni ngumu kutokea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.