Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs Ange Postecoglou amesema usajili wa kiungo wa kimataifa wa Uingereza James Maddison ulifanyika kwa wakati sahihi katika dirisha lililopita.
Kocha Ange amesema alimuona mchezaji huyo na kuvutiwa nae na kumuhitaji na klabu ilimpa ushirikiano mapema na kufanikiwa japo kuna vilabu kadhaa pia vilikua vikifukuzia saini ya mchezaji huyo.Kiungo James Maddison mpaka sasa ameshafanikiwa kuhusika kwenye mabao manne katika michezo minne aliyofanikiwa kucheza ndani ya Tottenhan ambapo amefunga mambao mawili na kuisaidia upatikanaji wa mabao mawili.
Kocha Ange anasema kusajiliwa kwa Maddison ni jambo ambalo limefanywa wakati muafaka kwani mpaka sasa mchezaji anaonekana namna ambavyo analeta athari chanya ndani ya timu hiyo akishirikiana na wenzake.Kiungo James Maddison amekua na mwanzo mzuri ndani ya klabu ya Tottenham kama klabu yake pia ambayo imekua na mwanzo mzuri kwenye ligi kuu ya Uingereza, Hii ikidhihirisha maneno ya kocha Ange Postecoglou