Ramsdale Amsifu Maguire

Golikipa wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza Aron Ramsdale amemsifu mchezaji mwenzake wa timu ya taifa beki Harry Maguire kutokana na uwezo wake wa kuvumilia ukosoaji unaofanywa kwake.

Ramsdale amemsifu Maguire kwa kuendelea kua bora licha ya kukosolewa mara kwa mara na mashabiki wa timu yake kuanzia klabu yake ya Man United mpaka timu ya taifa ya Uingereza.ramsdaleBeki huyo alipata ukosoaji mkubwa katika mchezo wa Uingereza uliopita dhidi ya Ukraine na mashabiki wa klabu hiyo, Ikiwa inaelezwa ndio sababu ya kocha Southgate kumpumzisha katika mchezo wa jana dhidi ya Scotland.

Golikipa Ramsdale wakati anazungumza na wanahabari baada ya mchezo wa jana dhidi ya Scotland anasema Maguire amepokea ukosoaji kwa miezi 18 nyuma na haijamuathiri na ameendelea kua bora na ndio sababu anaendelea kuitwa timu ya taifa.ramsdaleBeki Maguire amekua akiandamwa na mashabiki wa timu yake kutokana na makosa ambayo amekua akiyafanya mara kwa mara, Lakini kocha wa timu ya taifa Gareth Southgate anaamini kwenye ubora wa beki huyo licha ya ukosoaji anaopitia.

Acha ujumbe