Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos ambaye alikua anaifundisha timu ya taifa ya Poland amefutwa kibarua cha kuinoa timu hiyo shirikisho la soka nchini Poland limethibisha.
Kocha Fernando Santos ameanikiwa kuiongeza timu ya taifa ya Poland kwenye michezo sita tu lakini shirikisho la soka nchini humo limeona kocha huyo hatoshi kuinoa timu hiyo na kuamua kumtimua.Kocha huyo wa zamani wa Ureno ikumbukwe alifutwa kazi na timu ya taifa ya Ureno baada ya timu hiyo kutolewa kwenye hatua ya robo fainali ya kombe la dunia nchini Qatar mwaka jana na Poland wakaamua kumpa kibarua.
Katika michezo sita ambayo kocha huyo ameiongoza Poland alifanikiwa kushinda michezo mitatu na kufungwa hivo asilimia za ushindi zilikua ni 50 na kupoteza ni 50, Lakini haikuwashawishi Poland na kuamua kumtimua kocha huyo.Kocha Fernando Santos pamoja na kutimuliwa na Poland kama ilivyokua Ureno mwezi Disemba mwaka jana, Lakini atakumbukwa kama kocha pekee aliweza kuwapa Ureno taji la kwanza katika historia ya nchini hiyo mwaka 2016 walipobeba taji la mataifa ya ulaya.