MABONDIA WATATU KUPANDA ULINGONI KUIWAKILISHA TANZANIA LEO

Bendera ya Tanzania 🇹🇿 itapeperushwa tena usiku wa leo usiku kwenye hatua ya robo fainali mashindano ya kufuzu Olimpiki ya Paris 2024 kwa Bara la Africa ambapo mabondia 3 watapanda Ulingoni.

Pambano la kwa Tanzania litakua katika bout no. 165 uzani wa 66kg ambapo Malkia wa Ngumi Tanzania na mshindi wa medali ya fedha Ubingwa wa Afrika 2023 atapambana na bondia maarufu Imane Khelif kutoka Algeria.

Katika bout no. 166 uzani wa 51kg bondia machachari Abdallah Abdallah “KATOTO” atapambana na Said Mortaji kutoka Morocco.

Na pambano la 3 kwa Tanzania “Faru weusi wa Ngorongoro” la bout no. 170, Nahodha wa timu ya Taifa na mshindi wa Medali za Shaba Ubingwa wa Afrika 2023 na Jumuiya ya Madola Birmingham 2022, Yusuf Changalawe atapanda ulingoni dhidi ya Seydina Konate mwenyeji kutoka Senegal.

Awamu ya mapambano haya yataanza rasmi muda wa saa 2.00 usiku na yatarushwa mubashara kupitia livestream channel ya IOC.

Mungu wabariki Mwakamele, Abdallah “Katoto” na Changalawe

Acha ujumbe