Klabu ya Liverpool imeingia jumla kwa kiungo wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Uholanzi Ryan Gravenberch wakihitaji saini ya kiungo huyo.

Taarifa zinaeleza kua Liverpool wapo kwenye mazungumzo na Bayern Munich juu ya kiungo huyo na kinachojadiliwa zaidi ni kiwango cha pesa na kama itaonekana kiwango kinafaa basi hatua zingine zitafata.liverpoolHii inaonesha bado Vijogoo wa Anfield hawajamaliza kuisuka safu yao ya kiungo ndani ya msimu huu na ndio sababu wanamuhitaji Gravenberch kwa uhamisho wa kudumu aje aongeze nguvu kwenye safu ya kiungo ya klabu hiyo.

Kiungo Ryan Gravenberch inaelezwa amekubali kujiunga na klabu ya Liverpool na kinachosubiriwa ni makubaliano baina ya vilabu ili kumruhusu kiungo huyo akakipige kunako ligi kuu ya Uingereza msimu huu.   liverpoolKiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekua hafurahishwi na yeye kukosa nafasi ndani ya klabu ya Bayern tangu ajiunge klabuni hapo akitokea Ajax, Hivo ameona akatafute changamoto nyingine nje ya klabu hiyo akiamini atapata muda wa kucheza zaidi.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa