Kuelekea mechi ya Manchester City na Leicester United, Liverpool wapo katika maombi mazito kuwaombea Manchester City kupoteza mechi yao ya leo. Ushindi wa Manchester City ni kujitangazia ubingwa ndani ya ligi hiyo kwa awamu ya pili ikiwa hata msimu uliopita walinyanyua ubingwa huo.
Mechi ya leo ni muhimu zaidi kwa Manchester City na ni zaidi ya fainali kwake kutokana na uhitaji wake wa kombe hilo la ligi. Matumaini ya Liverpool yameshikiliwa na Leicester ambao hawana cha kupoteza ndani ya mechi hiyo zaidi ya kukamilisha ratiba na kumzuia City kupata ushindi.
Hakuna shabiki wa soka mwenye mapenzi ya dhati na Liverpool anayetamani mechi ya leo impe ushindi mpinzani wake huyo na ni siku ambayo kwa hakika Leicester anakuwa na mashabiki wengi zaidi ya ilivyo siku zote ndani ya ligi kuu hiyo. Hilo linatokana na uhitaji wa kombe alionao Liverpool msimu huu.
Hata matumaini yake ya kunyanyua kombe la klabu bingwa yapo uvunguni sana baada ya kuwa na deni kubwa la magoli mbele ya klabu ambayo ni bora sana msimu huu. Walipoteza mechi yao ya awali dhidi ya Barcelona ambao watarudiana hivi karibuni kwa idadi kubwa ya magoli.
Idadi hiyo kwa hakika inawakosesha nafasi kubwa ya kusonga mbele zaidi kwenye michuano hiyo ambayo kwa hakika walikuwa na njaa nayo sana kutokana na usajili alionao na kwa hakika haukutakiwa kabisa kumzuia kufanya vizuri zaidi kwenye michuano hiyo msimu huu.
Kwa sasa, baada ya kucheza michezo yake ndani ya ligi anazidi kumuombea njaa ndugu yake kupoteza mechi hiyo kubwa ya leo ambayo kwa hakika ni muamuzi wa mwisho kabisa wa ushindi wa kikombe hicho cha ligi kuu ambacho kimekuwa na upinzani wa aina yake.
Hii inamaanisha endapo Manchester City atapoteza mechi yake basi atakuwa amepoteza kabisa nafasi yake ya ushindi wa taji hilo na kumruhusu Liverpool kuondokana na njaa yake ya kipindi kirefu ya kukosa ubingwa wa ligi hiyo. Na kama atashinda mechi hiyo msiba wa Liverpool utaendelea kubaki palepale.
Ikiwa ni njaa ya klabu hiyo kunganyua kikombe hicho huku Pep naye akitaka kupigana ili angalau asionekane amemaliza msimu wake bila kuwa na kikombe chochote hivyo hilo linafanya ushindani kuwa mgumu sana kwa kipindi hiki cha mechi za mwisho kati ya klabu hizo mbili.

