Klabu ya Liverpool inamfukuzia kwa karibu kiungo wa klabu ya Rb Leipzig kutoka nchini Ujerumani Dominik Szoboszlai raia wa kimataifa wa Hungary ambaye anahitajika na majogoo ili kuimarisha kikosi chao.
Kuelekea msimu ujao klabu ya Liverpool inafanya sajili muhimu ili kukiboresha kikosi chao na kuhakikisha wanarudi kwenye ubora wao kwani msimu uliomalizika wamekua chini ya ubora wao ambao wamekua wakiuonesha miaka ya karibuni.Dominik Szoboszlai amekua na msimu bora sana ndani ya klabu ya Rb Leipzig jambo limeishawishi Majogoo kuhitaji saini mchezaji huyo, Taarifa zinaeleza majogoo hao wapo kwenye hatua nzuri ya kumchukua kiungo huyo.
Klabu ya Liverpool itakua imekamilisha usajili wa pili kama wakifanikiwa kunasa saini ya Dominik Szoboszlai kutoka Rb Leipzig, Akienda kua sehemu ya kikosi cha klabu hiyo kuelekea msimu wa mwaka 2023/2024.Liverpool wameshafanya usajili wa mchezaji mmoja mpaka sasa ambapo wamefanikiwa kumchukua Alexis MacAllister kutoka Brighton ambaye alikua kwenye ubora pia msimu uliomalizika, Hivo wakimpata na Szoboszlai itakua jambo zuri kwa klabu hiyo kuelekea msimu ujao.