Klabu ya Liverpool imeshikwa shati na klabu ya Brighton baada ya kulazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa katika dimba la Amex.
Liverpool sasa wanakua wamedondosha alama katika michezo miwili mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza, Mchezo uliopita walifungwa na Tottenham na leo wamesuluhu dhidi ya Brighton.Majogoo wa Anfield walitanguliwa katika mchezo huu ambapo Simon Andigra aliipatia Brighton bao la uongozi dakika ya 20, Kabla ya Mohamed Salah kufunga mabao mawili dakika ya 40 na dakika ya 45+1 na mchezo kwenda mapumziko Majogoo wakiwa mbele kwa mabao mawili.
Kipindi cha pili kilirejea klabu ya Brighton wakiwa na uchu mkubwa wa kusawazisha wakionekana kutengeneza nafasi za mara kwa mara,Huku vijana wa Klopp nao wakionekana kutafuta bao la tatu.Beki wa klabu ya Brighton Lewis Dunk alifanikiwa kuweka mzani sawa mnamo dakika ya 78 baada ya kuunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Solly March, Mchezo unamalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili na Liverpool wanadondosha alama mchezo wa pili mfululizo.