Klabu ya Arsenal wamefanikiwa kufuta uteja mbele ya klabu ya Manchester City baada ya kuifunga kwa bao moja kwa bila wakiwa katika dimba lao la nyumbani la Emirates.

Arsenal wameshinda dhidi ya Manchester City baada ya kupita kwa michezo 17 ambapo walipoteza michezo 16 ya nyuma, Hii inakua mara ya kwanza klabu hiyo kupata ushindi dhidi ya City tangu mwaka 2017.arsenalMchezo huo wa ligi kuu ya Uingereza uliopigwa katika dimba la Emirates ulikua wa tahadhari kubwa ambapo kila klabu ilionekana kucheza kwa umakini mkubwa ili kuepuka kutoa nafasi kwa mpinzani wake.

Mchezo huo ulikua wa kupokezana vipindi ambapo kipindi cha kwanza Man City walionekana kukitawala zaidi, Huku kipindi cha pili kikitawaliwa zaidi na washika mitutu kutoka jiji la London.arsenalGabriel Martinelli ambaye alitokea benchi akichukua nafasi ya Leandro Trossard ndio alieyepeleka kilio kwa klabu ya Manchester City,Ambapo dakika ya 86 ya mchezo aliifungia Arsenal bao ambalo ndio limewapa alama tatu vijana hao wa Mikel Arteta na kua ushindi wa kwanza dhidi ya City baada ya misimu saba.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa