Liverpool maarufu kama vijogoo wa Anfield walikumbana na dhahama katika usiku wa ulaya siku ya jumatano usiku katika dimba la Stadio Armando Maradonna.

Napoli katika ubora wao wakiwa katika dimba lao la nyumbani waliweza kuifunga timu ya Liverpool kwa jumla ya mabao manne kwa moja katika mchezo huo uliokua na kasi haswa upande wa Napoli ambao walionekana kua hatari zaidi katika mchezo huo.

Mchezo huo ambao wachezaji wa Liverpool walionekana kucheza kwa kiwango cha chini walinzi wake ambao waliigharimu timu hiyo kwa makosa binafsi na kusababisha timu hiyo kuadhibiwa kipigo hichi kikubwa.

napoliKwa upande wao Napoli walionekana kucheza kwa kiwango cha hali ya juu na kwa ushirikiano kama timu huku wachezaji kama Zambo Anguissa,Zielnski,pamoja Lobotka wakiwa mwiba mchungu kwa Liverpool.

Kwa upande wa kocha wa timu hiyo alipata nafasi ya kuongea baada ya mchezo huo na kusema hawakucheza vizuri ukizingatia siku tatu mbeleni wana mchezo dhidi ya Wolverhampton wanderers na kusema kwa walivyocheza jana timu hiyo itakua inacheka tu.

Na pale alipoulizwa kuhusu kufukuzwa kwa mjerumani mwenzake ndani ya Chelsea Thomas Tuchel vipi na yeye huenda akafukuzwa kwa matokeo mabaya anayoyapata hivi sasa Klopp alisema mabosi wake ni watulivu na wanatarajia mabadiliko kutoka kwake na sio mtu mwingine.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa