Luis Diaz Haendi PSG

Winga wa klabu ya Liverpool na timu ya Taifa ya Colombia Luis Diaz inaelezwa hana mpango wowote wa kujiunga na mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa klabu ya soka ya PSG.

Taarifa zinaeleza PSG haijafanya mazungumzo yeyote na klabu ya Liverpool juu ya winga huyo, Kwani kumeibuka uvumi kua mabingw ahao wa soka kutoka nchini Ufaransa walikua wanavizia huduma ya mchezaji huyo.luis diazUpande wa klabu ya PSG wao inaelezwa hawana mpango wowote wa kumsajili winga Luis Diaz na badala yake wana vipaumbele vingine kabisa ambavyo sio katika mchezaji huyo hii ikionesha kabisa klabu hiyo haina mpango na mchezaji huyo.

Upande wa klabu ya Liverpool nao unaelezwa hauna mpango wa kumuuza mchezaji huyo, Kwani wanamuona mchezaji raia wa kimataifa wa Colombia kama noja ya wachezaji muhimu zaidi klabuni hapo.luis diazWinga Luis Diaz amekua na kupanda na kushuka kipindi cha hivi karibuni na hii imekua ikichangiwa na majeraha ambayo amekua akiyapata, Lakini abdo haiondoi ukweli kua ni moja ya wachezaji muhimu kabisa ndani ya kikosi cha Liverpool.

Acha ujumbe