Baada ya Zinedine Zidane kurejea ndani ya viwanja vya Bernabeu zile habari za kumuwinda De Gea zimeanza kuchukua nafasi yake upya kwa mara nyingine tena. Hii inatokana na mapendeleo ya mwalimu wa kikosi hicho kwa sasa kutopendezwa sana na uwezo unaooneshwa na mlinda mlango aliyesajiliwa hivi karibuni kutoka Chelsea; Courtois ambaye anaonekana bado hajawa kwenye ubora wake.
De Gea amekuwa akihusishwa kujiunga na Madrid kwa kipindi kirefu sana tangu kocha huyo alipokuwa na kikosi hicho kwa mara ya kwanza kabisa. Lakini mipango hiyo ilisitishwa na wakamsajili mlinda mlango wa Chelsea, Courtois kama hatua ya mwanzo kabisa kusaidia kumpunguzia majukumu Navas pamoja na suala la umri wake kuanza kusogea.
Kutokana na mapendeleo hayo ya Zidane hata katika mechi yake ya kwanza alimuacha mlinda mlango huyo na kumuanzisha Navas. De Gea amekuwa akihusishwa na kujiunga na miamba hao wa soka Hispania na wao wameweka mezani donge nono ili kuwafanya United waweze kushawishika na kumuuza mchezaji huyo; kwa sasa wameweka chini kiasi cha £75m kama ada ya awali ili kumnasa.
Kumekuwa na sintofahamu juu ya mchezaji huyo kurefusha kandarasi yake klabuni hapo kwa sasa kitu ambacho kinaleta walakini kama mchezaji huyo bado ana nia ya kuendelea kusalia klabuni hapo au anaweza kuondoka. Lakini kila kitu huamuliwa na maamzi ya mtu na wakati endapo bado anawiwa kuitumikia klabu husika.
Japo katika siku za usoni baada ya Gunnar kuwepo kikosini hapo limeibuka suala linalowafanya wachezaji wengi warudi kwenye ari ya kuipigania timu yao. Ni suala lisilozuilika kwamba baada ya kuwasili kwa kocha huyo na kuanza kujenga historia mpya na timu hiyo imechangia kwa kiwango kikubwa sana kupatikana kwa matokeo uwanjani.
Japo matajiri wa klabu ya United wanaonekana kutoingiwa na wasiwasi juu ya mchezaji huyo na kwamba atasalia tu kikosini hapo bila shida yoyote na wameandaa donge nono la kumlipa katika mkataba wake unaoelekea kufikia kikomo. Kwa sasa wamemuwekea mezani £350,000 kwa wiki ili kumshawishi asiondoke klabuni hapo kama ilivyokuwa kwa Ronaldo ambaye walimuuza na baadaye wakajilaumu wenyewe kutokana na biashara yao hiyo waliyoifanya.
Kwa sasa klabu hiyo inajipanga kurudi kutoka kwenye kipindi kigumu walichotoka kupitia kwa kufanya usajili mkubwa ambao utaipa mafanikio klabu hiyo. Sio Julen Lopetegui wala Santiago Solari walioshindwa kuipa mbio za mafanikio Madrid lakini kwa sasa wana imani kubwa baada ya kurejea kwa kocha huyo aliyewapa mafanikio makubwa miamba hao wa soka kwa kipindi chake cha nyuma kabla hajaondoka.
Kwa sasa wameanza kuanika mezani majina ya baadhi ya wachezaji ambao wangetamani kuwashusha kikosini hapo wakiwemo Eder Militao kutoka Porto, Eden Hazard na Christian Eriksen bila kumuacha De Gea mwenyewe.


Asia Abdy
De Gea hana shuhul
Furahav
Huyu De anajua sana.
Povel
Da gea yupo vzr