Madrid ni Vitendo Tu!

Klabu ya Madrid tayari imeanza kukamilisha hesabu yao sokoni kwa kufanya usajili mapema kabla ya kuanza majaribio ya kikosi chao katika msimu huu wa likizo ndani ya ligi (kabla ya msimu mpya). Klabu hiyo imefungua pazia la kumsajili nyota ambaye alikuwa anahusishwa kwa kiasi kikubwa na klabu nyingi kubwa.

Luka Jovic kutoka klabu ya Frankfurt amekuwa na msimu wa pekee sana ndani ya kikosi hicho jambo lililompelekea kupata nafasi ya kandarasi ya kikosi cha Zidane ambaye anaonekana kuwa na umaana mzito wa kukisuka kikosi hicho baada ya kuwa na safari ngumu sana msimu huu.

Mara nyingi Madrid wakiridhika na mchezaji humpa kandarasi ya muda mrefu zaidi ili kuweza kumjengea imani ya kupambana kulipa uaminifu aliowekewa. Amesainishwa mkataba wa miaka sita ndani ya klabu hiyo ikiwa ni hatua ya mapema sana kuwa na mshambuliaji wa aina yake atakayeweza kukaa kwenye mipango ya Zidane.

Anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa ndani ya klabu hiyo huku kukiwa na watangulizi wengine ambao tayari wametua kikosini hapo wakiwemo: Eder Militao na Rodrygo ambao tayari majina yao yanatajwa na vyombo vya habari vya klabu hiyo kwa ajili ya kufanya maajabu msimu ujao wa ligi.

Makubaliano yote yamefanyika na kilichosalia ni hatua ndogo ndogo sana zikiwemo zile za vipimo ili kuweza kuona utimamu wa kimwili wa nyota huyo ambaye amegharimu kiwango cha £60m kumwaga wino ndani ya klabu ya matajiri hao wa soka barani Ulaya hususan Hispania.

Mbali na nyota huyo bado kuna mazungumzo yanaendelea kuwanasa Eden Hazard ambaye amekuwa kwenye rada kwa kipindi kirefu sana na mlinzi wa kushoto wa Lyon, Mendy ambao mawasiliano na makubaliano yanaendelea vizuri na kuna kila dalili wakatua kikosini hapo wakati wowote ule.

Kwa sasa hawana wasiwasi juu ya mbadala wa Benzema ambaye kwa sasa ndiye mchezaji tegemezi ndani ya kikosi hicho na umri wake ukiwa umesogea kiasi cha kupunguza kasi ya ushambuliaj lakini bado ana nafasi ya kuipeleka klabu hiyo mbali msimu ujao baada ya kupotea kwa muda. Hilo haliwezi kuzuia nafasi ya Jovic kucheza kwa sababu za kimfumo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.