Kila kocha anapokuwa katika klabu fulani kufundisha huwa na nia kubwa moja ya kutaka kufanya vizuri na kufahamika zaidi kwa matunda na kazi kubwa anayoifanya. Zaidi ya hayo huwa na nia ya kuonesha uwezo wake wa kufundisha soka na kila mmoja akaheshimu nafasi yake kiushindani.
Japo hutokea wakati ambapo kocha huyo anashindwa kufikia malengo ambayo klabu yake inayaweka au hata yeye mwenyewe anakuwa ameyaweka kwa kipindi chake akiwa kama mwalimu wa timu hiyo. Jambo kama hilo huwa gumu kuweza aidha kuvumilika kwa wamiliki au hata yeye mwenyewe kujishauri juu ya matokeo yake.
Baada ya hali hizo hupelekea kujishusha kabisa kiuwezo au watu wa pembeni ambao wanaangalia kile kinachofanywa kudharau nafasi hiyo kwa kuona kwamba sio nafasi yake kufanya vizuri kwenye nafasi hiyo. Jambo kama hilo humfanya kocha huyo aweze kuchukuliwa kawaida sana kiutendaji.
Mbali na hapo wafuatao ni baadhi ya makocha ambao wamekosa kabisa kuuza Ulaya pamoja na kufundisha soka lenye mvuto lakini nafasi yao kwa sasa inaonekana kama haipo kutokana na utawala wa warithi wao kufanya makubwa zaidi yaliyofunikwa na kile walichokifanya wao kwa kipindi chao chote:
Bruce Rioch, ili kutambua nafasi yake ni lazima kujiuliza swali hili: Klabu ya Arsenal iliongozwa na nani kabla ya Wenger? Jibu la swali hili litatupeleka moja kwa moja kutambua nafasi aliyokuwa nayo kocha huyo katika kipindi kukiwa na watu kama Ian Wright ndani ya ardhi hiyo ya Emirates. Lakini kwa sasa ni vigumu sana kukumbuka nafasi yake kutokana na kuwepo kwa Wenger ambaye amefuta kabisa uwepo wa mtangulizi huyo. Jambo hilo kwa hakika limempoteza kabisa mwalimu huyo na kuondoa uwepo wake kizazi cha sasa.
Alan Ball, mkongwe aliyezitumikia klabu za Southampton na Manchester City kwa kipindi chake cha kufundisha soka. Anakumbukwa kwa mfumo wake ambao alipenda kuutumia mara zote wa 4-4-2 ambapo ulionekana kuwa na matunda lakini kwa falsafa yake ulikuwa ni mgumu sana kupata matokeo. Miongoni mwa kitu hakiwezi kusahaulika kwake ni kwamba alikuwa ni mchezaji zaidi ya kocha kwa sababu akiwa kama mchezaji alifanya makubwa zaidi ya alipokuwa kocha.
Brendan Rodgers, alihudumu katika klabu kubwa nchini Uingereza na kuwa na matokeo mazuri sana lakini kwa sasa amesahaulika kabisa kuwa kama ni mtu ambaye ana historia kubwa. Hata kipindi cha uongozi wake hakupata heshima inayostahili sana kwa nafasi yake. Alifanya kazi akiwa kama kocha wa Swansea City na Liverpool na katika kipindi chake chote alifanya mazuri yanayofaa kusifiwa sana.


Povel
Gud news