Mapacha Wanaocheza Soka

Mara chache sana kukuta familia moja ya watoto wawili waliozaliwa pamoja kufanya kitu kinachoendana na kwa kiwango kile kile kinachooneshwa na mmoja. Lakini katika nchi za wenzetu ni kawaida sana kukuta mapacha wakiwa wanafanya jambo moja kwa kiwango kinachoendana kutokana na utamaduni wao wa kukiendeleza kipaji chao.

Kuna wengine hata kutokana na uwezo wao basi wameweza kukutwa wanacheza ndani ya klabu moja na kukusanya mafanikio ndani ya klabu hiyo hiyo jambo ambalo kwa hakika linaonesha mafanikio makubwa mno ndani ya soka. Leo tutakuletea baadhi ya mapacha wa kufanana wanaocheza soka la kulipwa Ulaya:

Rafeal na Fabio Da Silva, mapacha hawa wenye uraia wa Brazil waliweza kushinda kombe la ligi pamoja msimu wa 2010/2011 japo Rafael aliweza kushinda mawili akiwa kama mchezaji wa timu ya wakubwa ya klabu hiyo. Kuna hata wakati walikuwa wakipewa nafasi ya kucheza ndani ya mechi moja pamoja kutokana na kuaminiwa uwezo wao na kocha na hakuna kilichokuwa kinawazuia wawili hao kucheza ndani ya klabu hiyo.

Nazim na Kalim Amokachi, wachezaji wenye asili ya Kiafrika na raia wa Nigeria ambao waliweza kupata nafasi ya kuwika ndani ya ligi ya Uturuki wakiwa na klabu kongwe ya Besiktas. Wawili hao waliweza kupata nafasi ya kucheza pamoja ndani ya klabu hiyo na kwa hakika waliweza kuaminiwa kutokana na kiwango chao bora kabisa hata walipopewa majukumu uwanjani. Waliweza kuacha alama ndani ya ardhi hiyo.

Florentin na Mattias Pogba, hawa ni kaka zake wa damu na nyota wa Manchester United, Paul Pogba. Kwa hakika ni familia ya kipekee kutokana na watatu hawa wote kuwa wachezaji wa soka wenye uwezo wa pekee sana. Wawili hao wamekuwa wachezaji wa St. Etienne tangu mwaka 2012 na wamecheza ndani ya klabu hiyo kwa mafanikio makubwa sana. Kwa hakika ni mapacha wanaotuonesha kwamba katika maisha kila jambo likiwekewa nguvu linawezekana.

Marouane na Mansour Fellaini, wawili hawa ni maarufu lakini Marouane ni maarufu zaidi kutokana na historia yake kubwa katika soka. Akiwa katika maisha yake ya soka amepitia vilabu vikubwa ikiwemo Everton na Manchester United. Lakini wawili hawa kwa hakika ni wachezaji wakubwa wenye uwezo wa kipekee na ni miongoni mwa mapacha wenye historia kisoka.

Rogelio na Ramiro Funes Mori, wote hawa wanajihusisha na soka lakini katika vilabu tofauti. Ramiro akiwa ni kiungo mkabaji anayekipiga klabu ya Everton huku ndugu yake huyo akiwa anakipiga katika klabu ya C.F. Monterrey huko Mexico.

2 Komentara

    Duh thnks kwa information

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.