Man United Mawindoni, Chaka Kwa Chaka.

Wakati mashindano ya Euro 2020 yakiendelea, ni dhahiri baadhi ya vilabu vinayatizama mashindano haya kwa jicho la tatu, Man United wapo mawindoni, chaka kwa chaka.

James Rodriguez aling’aa kwenye Kombe la Dunia 2010 na baadae akasajiliwa na Real Madrid baada ya mashidano yale. Huu ni mfano tu, kwenye Euro kuna kinda wa PSV – Denzel Dumfries (Uholanzi) ama hakika kwa timu zinazotafta beki wa kulia, hii ni nyota inayong’aa.

Tukirudi Uingereza, Man United inayatizama mashindano ya Euro 2020 kwa jicho kubwa zaidi. Kieran Trippier na Jadon Sancho wanaangaliwa na kutafatwa kwa udi na uvumba na vigogo wa Old Trafford. Ofa za awali kupelekwa Atletico Madrid na Dortmund, zote ziligonga mwamba, United wanarudije? Watafanikiwa kwenye chaka la uingereza?

Kwenye machimbo ya Hispania, United wanahaha kunyakua walinzi wa Madrid. Sergio Ramos yupo sokoni kama mchezaji huru lakini macho ya Ole Gunnar Solskjaer yanamtizama Rafael Varane zaidi.

Real Madrid wameweka dau la £80M kumsajili Varane wakati ambapo United wametoa £50M pekee. Inasemekana, Man United ipo kwenye mazungumzo na wakala wa Varane katika kuhakikisha mchongo unakamilika wakati huu ambao beki huyu amekataa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Santiago Bernabeu.

Hakika Man United wapo mawindoni, chaka lipi litamtoa United kimasomaso au atakwama njiani na kuambulia patupu?


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe