Pogba Kukamata £400000 Hadi 2026

Manchester United inaripotiwa kujiandaa kumpa Paul Pogba kmkataba wa miaka mitano wen ye thamani ya Pauni 400,000 kwa wiki, ambayo itamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye miaka 28 na Mashetani Wekundu unatarajiwa kumalizika Juni mwakani, na vilabu kadhaa, wakiwemo Paris Saint-Germain, Real Madrid na Juventus, vinaendelea kuhusishwa na saini yake.

Wakala wa Pogba Mino Raiola anadaiwa kuwa alifanya mazungumzo na PSG wiki iliyopita juu ya uwezekano wa kuhamia mji mkuu wa Ufaransa katika msimu huu wa usajili wa majira ya joto.

Wakati huo huo, ripoti ya hivi karibuni ilidai kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa bado ana nia ya kuhamia Real Madrid licha ya Zinedine Zidane kuondoka.

Hata hivyo, kwa mujibu wa The Sun, Man United wana hamu kubwa ya kusalia na mshindi huyu wa Kombe la Dunia, ambaye kwa sasa anaiwakilisha nchi yake kwenye Euro 2020.

Ripoti hiyo inadai kwamba mabingwa hao 20 wa Uingereza wanapanga kumpa kiungo huyo kandarasi ya miaka mitano yenye thamani ya Pauni 400,000 kwa wiki, ambayo itampeleka hadi msimu wa joto wa mwaka 2026.

Upande wa Ole Gunnar Solskjaer unatajwa kuwa tayari kusubiri hadi baada ya Mashindano ya Kimataifa ya Uropa ili kumalizia majadiliano lakini wanataka makubaliano hayo yafanyike kabla ya kuanza kwa msimu ujao.

Pogba, ambaye kwa sasa anapata pauni 300,000 tu kwa wiki, alifunga magoli sita na kutoa usaidizi wa magoli tisa katika mechi 42 za Man United wakati wa kampeni ya 2020-21.


 

USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.