Mshambuliaji wa England Raheem Sterling amekiri kuwa hakuwa na furaha kwa kukosa mda wa kutosha wa kucheza huko Manchester City msimu uliopita.
Sterling amehusishwa na kuondoka kwa mabingwa wa Ligi Kuu baada ya baada ya kuhudumia benchi mara kadhaa mwishoni mwa kampeni ya 2020-21, pamoja na robo fainali ya Ligi ya Mabingwa na pia nusu fainali.

Lakini mchezaji huyo wa miaka 26 amekuwa mtu muhimu kwa Uingereza katika mechi zao za ufunguzi za Mashindano ya EURO 2020, akifunga bao la ushindi dhidi ya Croatia wiki iliyopita.
Akizungumzia hali yake ya soka wakati wa kuelekea kumaliza msimu, nha hali ya kukosa mda wa kutosha wa kucheza, staa huyu anasema;
“Ikiwa huchezi, huna furaha. Ni mimi, huyo ni mimi tangu nilipokuwa mtoto, ikiwa ninacheza mpira nina furaha sana, ikiwa sichezi sina furaha.”
-Raheem
Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao


