klabu ya Man United inaelezwa kufikia pazuri na golikipa wa klabu ya Inter MIlan ya nchini Italia Andre Onana kwajili ya kumsajili kipa huyo kujiunga na mashetani wekundu.
Man United wanaelezwa kufanya mazungumzo na golikipa huyo binafasi na raia huyo wa kimataifa wa Cameron ameonesha nia ya kujiunga na klabu hiyo, Huku Mashetani wekundu wakitarajiwa kufanya mazungumzo na klabu ya Inter Milan leo.
Taarifa zinaeleza kua klabu hiyo inatarajiwa kutuma ofa yake ya kwanza baada ya mazungumzo usiku wa leo kwa klabu ya Inter Milan, United wanatajwa kuhitaji saini ya golikipa huyo haraka iwezekanavyo ili kujiandaa na msimu mpya.
Man United wanatarajiwa kuachana na golikipa wake mkongwe ambaye amekua kwenye ubora mkubwa miaka 12 aliyoitumikia klabu hiyo David De Gea, Hivo wanahitaji golikipa mpya kwa haraka kwajili ya kuziba nafasi ya De Gea.
Klabu ya Man United wanaelezwa wanataka kuhakikisha dili la Onana linakamilika mapema sana kabla hata ya maandalizi ya msimu kuanza, Kwani kocha Erik Ten Hag anahitaji kupata wachezaji wake muhimu mapema ili kuandaa timu ya ushindani kuelekea msimu ujao.

