Manchester City walishindwa kutetea ubingwa wao msimu uliopita, wakati Liverpool wakilitia mikononi taji la Ligi Kuu baada ya miaka 30 ya kusubiri. Kibarua walichonacho mkononi kwa sasa ni kurejesha taji walilopoteza msimu uliopita.
Msimu huu umeanza vyema Manchester City pale Molineux baada ya kumuacha mwenyeji wake Wolverhampton kwa kichapo cha bao 1-3.
Mechi hii ilikuwa ngumu kwa wenyeji, huku wageni kimahesabu wakiucheza mpira mwingi na mashambulizi.
Safari ya ushindi ya Man City ilianzishwa na goli la Kevin De Bruyne dakika ya 20 baada ya kuona nyavu kwa penati, kabla ya Phil Phoden hajachungulia nyavu kuongeza goli la pili dakika ya 32.
Paul Jimenez wa Wolves alijaribu kuwafuta machozi kwa goli la kwanza na la mwisho kwa timu yake dakika ya 78, huku Gabriel Jesus akipigilia msumari wa 3 kwa Manchester City.
Inakumbukwa, Wolves alimchapa City nyumbani na ugenini kwa msimu uliopita, bila shaka City hawakupenda kuanza kibarua kwa aibu, na ushindi huu ni mwanzo wa matumaini kuelekea kutetea taji walilolipoteza.
Bila shaka City walijifunza kwa vichapo vya nyumbani na ugenini msimu uliopita na hawakutaka kurudia makosa, washindani wao Liverpool wameshacheza mechi mbili na zote wameandika ushindi.
FURAHIA KASINO YA MTANDAONI
Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.


magdalena
city wakikazana vya kutosha na juhudi za hali ya juu wanaweza pata ubingwa msimu huu
Ernest
Kinachofuata sasa ni kila mtu ashinde mechi zake
Elika
Hapo sasa ndo penyewe
Tatu
Man city awakutaka kuludia makosa Yale yale tena kichapo alichokipa nyuma Mfulizo walijipanga vema
Shan
Msimu umeanza vyema kwa man chester
Dorophina
Man City msimu huu inatakiwa wapambane warudishe taji nyumbani
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri Sana kinacho fata Sasa kila mechi watoke naushindi wa kupambana
Zeiyana
Ndio walivyo man city wanaazaga vizuri mwisho wasiku akuna kinacho endelea
Caroline
Sema hii mechi ulikua ngumu Sana jmn.wamejitaidi mno
Angelina
Mancity msimu huu wamekuja kivingine
Antony Luseno
Ukiachilia kuwa na wachezaji wazuri pia wana kocha mzuri ambaye ni kocha wa matokeo
Neema
Habarii njema sana hii
Amani
Mancity msimu huu wamekuja kivingine Liverpool wajipange
Sadick
Ulikuwa ushindi mno kutoka kwa mpinzani ambae msimu uliopita alifungwa mechi zote#meridianbettz
Salma ngende
Mambo mazuri hayo
Gabriel
Manchester city wameanza vizur sana 👍
Venerose
Manchester msimu huu Kama mtafanya vizuri
jullie
hongera zao bwana
Hopemwaikuka
Nimeona juhudi zao Ila wakaze ndo kwanza kunakucha
Hidaya
City wakaze tu
Ester jackson
Msimu huu hakuna timu inayotaka kufanya vibaya ila ni mokosa ya mchezaji mmoja mmoja
Issa
City ni kama wamelipiza tu kwa wolves
lombo
saf
aisha
City safari hii wako vizuri sana
Amiri Kayera
Wameanz na moto
Rehema
Wako vizuri sana
Saupha mohamed
Good news
Sabrina
Man city wamekuja kwa kasi zaid
felister
hapo sasa ndo patamu
Mwanahamisi
Mambo mazuli hayo
Sauda
City wakaze buti
Frank P
Stil naona city kwa chelsea hatoboi msimu huu
Mwajumah
Mechi ilikua ngumu sana hii
Fatina
Safii
David Pere
Kinachofuata sasa ni kila mtu ashinde mechi zake