Manchester United Kujitafuta Dhidi ya Galatasaray Leo

Klabu ya Manchester United leo itashuka dimbani dhidi ya klabu ya Galatasaray katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya, Wakijitafuta baada ya kua na mwanzo mbaya wa msimu.

Manchester United itakwenda kucheza mchezo wake wa pili wa ligi ya mabingwa dhidi ya mabingwa hao wa Uturuki, Ambapo mchezo wa kwanza walishaupoteza dhidi ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani.manchester UnitedMan United mpaka sasa msimu huo umekaa vibaya kwakua wameuanza vibaya haswa kunako ligi kuu ya Uingereza ambapo wametoka kupoteza mchezo wao wikiendi iliyomalizika dhidi ya klabu ya Crystal Palace.

Mchezo wa leo wa ligi ya mabingwa ulaya unaweza kutoa dira kwa mashetani wekundu katika michuano hiyo, Kwani kama watashinda mchezo huo inaweza kuwaweka katika mazingira mazuri lakini wakipoteza itaendelea kuwaweka kwenye mazingira mabaya.manchester UnitedManchester United wanatakiwa kuamka usingizini mapema kwani wameshapoteza michezo mitano mpaka sasa kwenye michuano yote, Huku minne ikiwa ya ligi kuu ya Uingereza na mmoja wa ligi ya mabingwa ulaya jambo ambalo limekua baya sana kwa upande wa klabu hiyo hivo mchezo wa leo dhidi ya Galatasaray ni muhimu sana.

Acha ujumbe