Mshambuliaji wa zamani wa klabu za West Ham na Stoke City Marko Arnautovic amekataa offer ya kujiunga na klabu ya Manchester United baada ya kuonesha nia ya kutaka huduma yake msimu huu.
Klabu ya Manchester United ilitoa offer inayokadiria kufikai kias cha £7.6milion kwa klabu ya Bologna kwa ajiri ya mshambuliaji huyo ili aweze kurejea tena kwenye ligi kuu ya uingereza kabla ya mchezaji mwenyewe kukataa.

“Sifwati majina kwa sababu nadhani kwenye hii Pre-season wachezaji 250 walihusushwa au kutaka kujiunga na Manchester United, hivyo ndivyo ilivyokuwa .Tunawashambuliaji wawili, pengine wa tatu ni Marcus Rashford pia.
“Tunamchukullia kama mshambulilaji japo amekuwa kwenye kiwango kizuri kwenye pre-season kwenye upande wa kushoto na leo alikuwa na nafasi nzuri mbili akitokea kushoto.
“Nafikili yalikuwa maamuzi sahihi kufanya hivyo. Lakini hatukuwa na namba 9 asilia leo.” Ten Hag bada ya mchezo wa leo kuisha alinukuliwa
Mpaka sasa Ten Hag amewezea kufanya sajiri sehemu ya kati na ulinzi, lakini bado hajafanikiwa kuboresha safu yake ya ushambuliaji, na kwa sasa anamuona Marko Arnautovic kama mtu sahihi wa kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji wa klabu hiyo.

