Klabu ya Manchester United imekamilisha usajiri wa mlinzi wa kimataifa kutoka nchini Argentina anayekipiga kwenye klabu ya Ajax Lisandro Martinez kwa uhamisho unaokaribia 57 million pounds.

Lisandro Martinez amejinga na Man United kwa kandarasi ya miaka mitano huku pia kukiwa na kipeengere cha kuongeza mwaka mmoja zaidi kwenye kandarasi na inatarajiwa kufikia tamati 2027.

Manchester United, Manchester United Wakamilisha Usajiri wa Lisandro Martinez, Meridianbet

“Ni heshima kwangu kujiunga na klabu hii bora, nimefanya kazi kubwa kwa ajiri ya kipindi hiki, na sasa naendelea kufanya zaidi na zaidi.

“Nimekuwa na bahati kuweza kuwa sehemu ya mafanikio ya timu ya Ajax kwenye kazi yangu, na hicho ndicho ninachotaka kukiendeleza Manchester United.

“Kuna kazi kubwa ili uweze kufika kwenye wakati huu, lakini naamini niko imara kwa hilo, chini ya kocha huyu na timu kwa pamoja tunaweza kufanikisha hilo.” Alisema Martinez kwenye mtandao wa Manchester United.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa