Klabu ya Man Utd imekataa mpango wa kubalishana wachezaji na klabu ya Atletico Madrid ambapo walihitaji kumtoa nyota wao wa kimataifa kutoka Ufaransa  Antoine Griezmann ili waweze kumpata Cristiano Ronaldo.

Cristiano Ronaldo anahitaji kuondoka kwenye klabu  ya Man Utd ili aweze kupata nafasi ya kucheza michuano ya ligi ya mabingwa ulaya, licha ya kurejea klabuni hapo siku ya Jumanne kwenye viwanja vya Carrington huku akisindikizwa na wakala wake Jorge Mendes lakini bado hatma yake haijulikani ndani ya klabu hiyo.

Man Utd, Man Utd Hawana Mpango wa Mabadilisho kwa Ronaldo, Meridianbet

Atletico Madrid wanahitaji kumpunguza Antoine Griezmann kwenye payroll ya klabu hiyo, Griezmann alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo akitokea Barcelona kwenye majira ya kiangazi, lakini kwenye makubaliano waliyoingia kati ya klabu hizo mbili ni Atl Madrid wanapswa kumnunua kabla ya june 2023.

Klabu ya Manchester wanatambua kuwa Atl Madrid wako tayari kumtoa Griezmann kwa mkopo kwenda kwenye klabu hiyo lakini hawataki kubadilishana na Ronaldo, japo walishawai kujaribu kumsajiri mchezaji huyo mara kadhaa.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa