Mlinda mlango wa klabu ya Leicester City Kasper Schmeichel ampenga kuachana na klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa takribani miaka 11  huku taarifa zikisema kuwa tayari ameshakubaliana na klabu ya nchini Ufaransa.

Golikipa huyo wa kimataifa kutoka nchini denmark mwenye miaka 35  kwenye miaka 11 aliyoitumikia klabu ya Leicester ameisaidia klabu hiyo kuchukua ubingwa wa EPL na FA Cup.

Schmeichel, Schmeichel Kuachana na Leicester, Meridianbet

Schmeichel amebakisha mwaka mmoja kwenye kandarasi yake na klabu ya Leicester na mpaka sasa bado hajafikiana makubaliano yoyote ya kandarasi mpya na klabu hiyo.

Kulinga na taarifa kutoka L’Equipe, Kasper tayari kashefikia makubalino na klabu ya Nice kujiunga na klabu hiyo kwenye dirisha la usajiri wa majira ya kiangazi hili.

Leicester City ndio klabu pekee kwenye ligi kuu ya Uingereza ambayo mpaka sasa haijafanikisha usajiri wowote.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa