MWENYEKITI wa Simba,Hassan Dalali pamoja na mwenyekiti wa mashabiki wa Simba Hamisi Kisiwa wameendela kukomaa kuwa Yanga hawawezi kuwa na sifa ya Unbeaten kwa sababu wamedroo mechi nyingi na kupelekea kupoteza sifa hiyo.

Hayo waliyasema wakati wa uzinduzi wa tawi jpya la Simba Mpira na Mipango lilipo Mbagala Kichemuchemu, ambalo lilifunguliwa wikiendi iliyopita na wazee hao wakiwa ni wageni waalikwa.

SImba
SImba

Wote kwa pamoja waligusia juu ya mashabiki hao kuhakikisha wanakua karibu na timu wakati huu ambao msimu mpya unatarajia kuanza. Huku wakiwa na Imani ya kuwa msimu ujao heshima itarejea.

Kisiwa alisema: “Bahati  nzuri mimi ni wa hapa hapa Mbagala tangu 2014 kwa hiyo shughuli imepata mtu sahihi, nafurahi sana kuwa hapa, niwape historia fupi ambayo wengi hawapendi kuisikia, lakini pai kwa faida ya vijana wa sasa na watoto.

“Ni mimi niliyeleta mfumo mzuri na sahihi kwa matawi kuwa msaada, nimekuwa mwenyekiti wa matawi yote Dar es Salaam kwa miaka 20, si jambo dogo, leo unaona ulivyo ustawi wa matawi, niwaombe tawi hili la Mpira na Mipango na iwe kweli.

Kwa upande wa Mze Dalali alisema:“Kuna watu wanasema wamevunja rekodi ya kuchukua ubingwa bila kufungwa, sio sahihi, wamedroo mechi tisa, Azam ili droo mechi saba, sisi tulidroo mechi mbili, rekodi gani imevunjwa hapo? Hakuna.

Simba
Simba

“Lakini pia niwapongeze viongozi wangu wa sasa wa klabu wanafanya mambo nzuri, usajili mzuri, tunakwenda kufanya vizuri, lakini ile sherehe yetu ya Simba Day niliyoanzisha mimi inakwenda kufanya tena wakati huu,” alisema.

Kwa upande wa Kisiwa mbali na kufungua tawi ukiwamo upandisha bendera, kukata uTepe wa ofisi, pia aligawa kadi za uanachama kwa Wanachama zaidi ya 50 wakiongozwa na mwenyekiti wao, Hamisi Ally.

 


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa