KIKOSI cha Simba kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki kesho jumatano dhidi ya klabu ya Haras El Hodoud inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri.

Simba vs Haras El Hodoud ni mchezo wa tatu wa kirafiki kwa hiyo kutoka nchini Tanzania tangu imetua nchini Misri kwa ajiri ya kuweka kambi ya kujiandaa na nichezo ya ligi kuu ya tanzania na mashindano ya kimataifa yanayotarajia kuanza hizi karibuni.

SIMBA, Simba Kucheza na Waarabu Kesho, Meridianbet

Simba iliondoka nchini Julai 14 mwaka huu, kuelekea kwenye mji wa Ismailia nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi na kujiandaa na michezo ya msimu ujao wa 2022/23.

Tayari kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mkuu, Zoran Maki kimecheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu ya Ismaily (1-1) na Al Akhdood (6-0).

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa