Mchezaji nyota wa klabu ya Mtibwa Sugar Baraka Majogoro amejiunga na klabu ya KMC  kwa uhamisho huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu hiyo  kwa msimu wa 2022/23 ataitumikia klabu ya KMC.

Baraka Majogoro amejiunga na KMC akitokea Mtibwa Sugar baada ya mkataba wake kumalizika na klabu hiyo kuamua kutomuongezea mkataba mwingine.

KMC, KMC Yamvuta Majogoro Kutoka Mtibwa Sugar, Meridianbet

Akizungumzia hilo, Baraka Majogoro alinukuliwa akisema kuwa “Nimesaini mkataba wa kukitumikia kikosi cha KMC baada ya mkataba wangu na Mtibwa kumalizika.

“Nina furaha sana kujiunga na timu hii na ninawaahidi kufanya kazi nzuri hivyo watarajie mambo mazuri kutoka kwangu.”

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Tanzania mwenye miaka 26, amevichezea vilabu vya Tanzania Prison, Ndanda, Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa