Golikipa namba moja wa klabu ya KMC Juma Kaseja bado ataendelea kuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo licha ya kuwepo kwa tetesi kuwa yupo kwenye listi ya wachezaji ambao klabu hiyo imapanga kuachana nao kwenye dirisha hili la usajiri

Baada ya kusambaa kwa tetesi kuhusu golikipa huyo kuachwa kwenye kikosi cha KMC,  uongozi pamoja na kaseja wametoka hadharani kukanusha taarifa na kuthibitisha kuwa golikipa huyo bado yupo kwenye kikosi cha timu hiyo na ataendelea kuwepo.

Kaseja, Kaseja Bado Yupo Sana KMC, Meridianbet

Kaseja amekuwa kipa mzawa mwenye ubora wa hali ya juu licha ya kwamba kwa msimu ulioisha hakupata nafasi sana.

Akizungumzia hilo, Walter Harrison amesema kuwa “Kaseja bado ni mchezaji wetu na amekuwa mfano ndani ya timu hivyo hatuwezi kumuacha.

“Wapo wachezaji ambao tumewaacha lakini Juma bado yupo sana KMC hata kama hatakuwa mchezaji lakini tutamtafutia hata nafasi nyingine.”

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa