Tayari Polisi Tanzania imeanza rasmi kambi yao kwa maandalizi ya msimu wa ujao jijini Dar es Salaam huku ikitarajia kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita.

Polisi, Polisi Tanzania Iko Chini ya George Mketo Sasa, Meridianbet

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa, wapo tayari kwa msimu mpya na wanaamini watafanya vizuri zaidi.

“Kikosi kimeingia kambini Jumatano hapa Dar na tutakuwa hapo kwa muda wa majuma kadhaa na wachezaji wetu wale wa zamani na wapya tutaanza nao kazi.

“Kambi ipo chini ya benchi la ufundi likiongozwa na kocha msaidizi ambaye tupo naye baada ya kuachana na Kocha Malale Hamsin.

“Tunategemea msimu unaokuja tutakwenda kupambana na kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita na tutakwenda kuanza kutoa dozi mwanzo mwisho, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa