Katikati ya Simulizi ya Fransesco Totti wa watakatifu wa Roma liliingia jina la Juma Kaseja wa Kigoma. Huyu ni nyanda na yule kiungo. Huyu ni mmanyema tu wa pale Kasulu.

.
Wakati majonzi yakiendelea ndani ya Stadio Olimpico, kila mtu anasikitika ajuavyo. Nje ya uwanja lilikuja gari moja jekundu lenye chata za manispaa.
.
Mwanzoni hakuna aliyelijali sana, walijua tu hawa ni wasumbufu wa jiji wapo katika pilikapilika zao za kila siku. Labda wapo hapa kuhamisha kontena zao za bidhaa. Lakini haikuwa hivo. Leo walikuwa hapa kwa kazi tofauti
.
Alitokea mzee mmoja wa miaka kama sitini hivi, akashuka katika gari lake lililoongozana na hili la manispaa. Akapanda juu ya Tela na kudandia whinch iliyomnyanyua juu sana.
.
Ilimnyanyua juu sana, juu zaidi ya urefu wa kuta za Stadio Olimpico. Kisha akatulia zake kuangalia yanayoendelea ndani.

Akatazama mechi ikaisha, akatazama sherehe nzima ya kumuaga Totti, ilipomalizika na yeye akashuka na kudandia gari lake akaondoka zake.
.
Wakati wote watu waliacha shughuli zao wakimshangaa lakini yeye hakujali. Wengine walimuona kichaa lakini hakujali. Alichojali ni kuwa anamshuhudia shujaa wa Roma akimaliza kazi yake ndani ya Roma.

.
Alipanga kuingia uwanjani kama mashabiki wengine lakini alifika na kuambiwa tiketi zimeisha. Ndipo akakubali kuingia gharama ya kuwalipa manispaa ili tu auone mwisho wa Fransesco Totti. Pesa ni nini mbele ya heshima ya mtu aliyewatumikia kwa damu yake yote?
.
Baada ya kumshuhudia Juma Kaseja katikati ya milingoti kwa miaka mingi, ninasubiri siku atakayoamua kumaliza maisha yake na mpira. Nitakwenda kumuaga popote atakapokuwa.

.
Labda itakuwa kwa Mkapa, labda tutakuwa tunacheza dhidi ya Misri ya Mohamed Salah. Labda uwanja utakuwa umejaa na nitakosa tiketi. Nitafanya nini??

.
Nitageuka yule mzee wa Italia, nionekane kichaa na watu lakini nimuage Juma Kaseja baada ya safari yake ndefu.
.
Baada ya Siku hiyo nitasubiri siku moja niwasimulie wajukuu zangu mechi zake bora kuwahi kutokea. Kuanzia kwa Zamalek pale Misri, mpaka CECAFA pale Uganda. NITASUBIRI
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???



Saupha mohamed
Kaseja alikua zamani
Lydia Emmanuel Magoti
Nakuwerewa mzee wakaz ukoseagi kaseja
Issa
K juma kipa makin
warda
Habari nzuri sana
Rahmal
Nice
Adelta
Zamani sio sasa Hana jipya
Shakila mrope
Zamani alikuwa anatamba sio sasa
Sarah
Hana jipya juma kaseja
Chiku
Maneno nimeyaelewa
Tatu
Nyota ya kaseja imeshuka asikiki tena kama zamani
Dorophina
Kaseja alikuwa vizuri zamani saiz hasikiki hata
Hopemwaikuka
Ni ww tu
Angelina
Goodnews