Simulizi ya Kaze Inavyonikumbusha ya di Mateo

Usiku wa june 29 mwaka 2011 Chelsea ilimteua Roberto di Mateo kuwa kocha msaidizi wa nguli Andre Villas Boas, bila hiyana Roberto akakubali majukumu yale, Matokeo yasiyoridhisha yaliikumba Chelsea na hapo ndipo kocha mkuu Boas akafungashiwa virago.

March 4 2012 mabosi wa Chelsea wakakubaliana kua Roberto di Mateo awe kocha mkuu wa Chelsea bila ya kujali michuano migumu ya UEFA iliyoendelea. Mungu si athumani, di Mateo akaweza kuuvunja mfupa uliomshinda Villas Boas katika usiku wa raha pale Allianz Arena Ujerumani.

Ilikua vita ya fainali ya wababe wa London na wajerumani Bayern Munichen, Thomas Muller anaingia kambani na kisha Drogba anachomoa dakika ya 85. Fainali ngumu kweli kweli. Wanaume wakaingia extra time huku Arjen Robben anakosa penalti kisha extra time inasoma 1-1. Referee Pedro Proenca anaamua matuta ya penatI na Chelsea anachukua kombe la UEFA baada ya penati ya Drogba.

London yote ikaimba jina la Roberto di Mateo. Hali hii nimeanza kuiona kwa Cedric Kaze aliyeweza kutafuna mfupa uliomshinda Mwinyi Zahera, Luc Emeyl na Zlatko.

Sitosubiri afe ndipo nimpongeze, laa.. bali kwenye kila haki pana wajibu. Haki yetu ni kushangilia na kuzomea lakini ni muhimu kupongeza uwajibikaji. Nimeiona yanga mpya kabisa. Ni kama ile ya kampa kampa tena ya 2016, yanga ipo vizuri sasa.
.
Kaze amefanya kila shabiki wa yanga ajiskie raha mwaka 2020, mwaka unaisha vizuri kwao. Ligi imekua tofauti na miaka miwili nyuma. Inapendeza kwakweli. Ushindani ni mkubwa. Asante sana Cedric kaze kwa burudani.


.
Nimemuona Kaseke mpya, nadhani anayafurahia maisha yake pale yanga. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Historia ya di Mateo inaweza ikajirudia kwa Cedric kaze. Raha ya soka imerudi bongo. Record ya UNBEATEN inawaumiza kichwa makocha wengi.

14 Komentara

    Asante kwa simulizi hii

    Jibu

    Asante kaze kwa kutujuza

    Jibu

    Asante sana simulizi iko vizuri

    Jibu

    Hii ni makala nzuri yenye kiburudisho na maelezo mazuri

    Jibu

    Asante kwa taarifa meridian bert watu makini

    Jibu

    Makala safi

    Jibu

    Hinapendeza hii

    Jibu

    Kazi ya ukocha bwana nzuri ukishinda ngumu ukifugwa

    Jibu

    Asante kwa makala nzuli

    Jibu

    Tunashukur sana

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Habar nzur

    Jibu

    Goodnews

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.