Mason Mount Bado Yupo Majeruhi

Kocha wa Manchester Ruben Amorim amezungumza kuhusu kiungo wake raia wa kimataifa wa Uingereza Mason Mount kua bado hajawa fiti kurejea uwanjani kwakua bado anasumbuliwa na majeraha.

Kiungo Mason Mount alishindwa kumaliza mchezo wa derby dhidi ya Manchester City siku ya Jumapili baada ya kupata majeraha katika mchezo hu na kochga wake Amorim amezungumza kwa kusema mchezo huyo hatakuepo kwenye mchezo dhidi ya Tottenham leo kutokana na kusumbuliwa na majeraha, Ammbapo majeraha hayo yanaelezwa kumfanya ajiskie vibaya sana.mason mount“Hayupo, bado ana majeraha. Ana huzuni sana. Chumbani alikuwa na huzuni sana, sana, kwa hivyo tunahitaji kumsaidia.”

“Wakati mchezaji yuko kwenye hali kama hii na majeraha mengi na ratiba ngumu, inakuwa ngumu sana kwao.”

Mchezaji Mason Mount tangu ajiunge na klabu ya Manchester United mwaka 2023 amekua akiandamwa na majeraha mara kwa mara jambo ambalo limekua likimuumiza hata yeye kwani mpaka sasa hajapata nafasi ya kuonesha uwezo ndani ya kikosi hicho kutokana na majeraha ambayo yamekua yakimuandama, Lakini amekua akisisitiza atarejea kwenye ubora wake kwakua hata yeye mwenyewe anapitia kipindi kigumu sana.

Acha ujumbe