RAMOVIC AWATOLEA MACHO MASHUJAA

Saed Ramovic, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa baada ya kumaliza kazi kwenye mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo ni dakika 270 nguvu inaelekezwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex utakuwa ni wakwanza kwa timu hiyo kucheza ndani ya uwanja huo mpya kwa msimu wa 2024/25 katika mechi za ushindani kwa kuwa awali walikuwa wanatumia Uwanja wa Azam Complex.RAMOVICKwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 11 ndani ya ligi vinara ni Azam FC wenye pointi 33 baada ya kucheza mechi 15 ndani ya ligi.

Ramovic amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu hivyo wapo tayari kwa ajili ya kupambana kupata pointi tatu muhimu katika mchezo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tumetoka kucheza mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika huko ushindani ulikuwa mkubwa na sasa tunarejea kwenye ligi ambapo tuna mchezo muhimu dhidi ya wapinzani wetu ambao tunaamini kwamba wanahitaji pointi pia.

“Baada ya kumaliza mechi 3 za kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika sasa akili yetu ni kwenye ligi, tunataka kupambana na kupata pointi hilo linawezekana kwa kuwa tupo tayari.”

Acha ujumbe